0

Klabu ya Simba imetangaza kumtoa mzee Hamisi Kilomani kwenye Baraza la Wadhamini kwa kosa la kuvunja katiba ya klabu hiyo.

Pia, wanatarajia kumpekelea barua ya kumfuta uanachama na ikiwa hatafuta kesi na kushindwa kujitetea watamfukuza uanachama moja kwa moja.

Aidha, profesa Juma Kapuya ameteuliwa kuziba pengo la Ally Sykes ambaye kwa sasa ni marehemu katika baraza hilo, nafasi ya mzee Kilomoni imejazwa na Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Alhaj Adam Mgoyi.

KILICHOMPONZA HAMISI KILOMONI HIKI HAPA
Mwakilishi wa Baraza la wazamini wa klabu ya simba sc mzee Hamis Kilomoni , amefukwa uanachama na kupoteza sifa ya kuwa kiongozi au mwakilishi wa baraza la wazamini na badala yake nafasi yake imechukuliwa na Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Alhaj Adam Mgoyi wakati huohuo Professa Juma Kapuya anachukua nafasi iliyokuwa wazi baada ya Mzee Ally Sykes Kufariki, maamuzi haya yamefanyika leo tarehe 13 August 2017 kwenye mkutano mkuu wa wanachama wa simba sc uliofanyika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Conference Centre Dar es Salaam mbele ya wanachama.

Post a Comment

 
Top