Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema anavutiwa na winga wa Leicester, Riyad Mahrez lakini bado hajatuma maombi ya kumsajili nyota huyo.
Mahrez (26) amesaini mkataba wa miaka minne na Leicester mwezi Agosti, lakini tangu wakati huo amekuwa akiomba kuondoka klabu hapo.
Winga huyo alisaidia Leicester kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu wa 2015-16, kabla ya kumaliza nafasi ya 12 msimu huu.
"Je, tumetuma maombi kwake? Hapana. Hiyo siyo maana kwamba, hilo halitawezekana," alisema Wenger.
Mahrez alijiunga Leicester akitokea klabu ya Ufaransa ya Le Havre kwa gharama ya pauni 400,000 mwaka 2014 na 2016 alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa PFA.
Post a Comment