Khamis Mcha |
Klabu ya Azam FC imeendelea kujivua gamba baada ya kumtema rasmi mshambuliaji wake Khamis Mcha baada ya mkataba wake kumalizika.
Kuondoka kwa Mcha ni mwendelezo wa klabu hiyo kupunguza nyota waliokaa muda mrefu ndani ya kikosi chake hasa wale ambao mikataba yao inaelekea ukingoni.
Mbali na Mcha, timu hiyo pia imetangaza rasmi kuachana na mshambuliaji wake Ame Ali ambaye msimu uliomalizika alicheza kwa mkopo Kagera Sugar.
"Hawa wachezaji benchi la ufundi limetoa mapendekezo kuwa tusiwaongeze mikataba hivyo tayari tumeshawapa barua zao na tunawatakia kila la kheri huko waendako," alisema ofisa habari wa Azam FC, Jaffary Iddi
Post a Comment