0
 Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe  akipambana na mchezaji wa Madeama.

YANGA SC  imeshindwa kutamba kwa mara nyingine tena kwenye uwanja wa  nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Medeama SC ya Ghana katika mchezo wa Kundi A michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.

Donald Ngoma alianza kuifungia Yanga bao la kuongoza dakika ya pili ya mchezo huo akitumia vema makosa ya safu ya ulinzi ya Medeama na kuiweka timu yake mbele ya Medeama kwa bao 1-0.
Dakika 15 za kwanza watoto wa Jangwani walitawala mchezo kwa pasi za haraka huku wakiliandama lango la Medeama kitendo kilichosababisha wapate kona kadhaa.
Donald Ngoma akishangilia baada ya kuifungia Yanga bao.
Medeama walisawazisha bao hilo dakika ya 17 baada ya Bernard Danso kuunganisha mpira wa kona na kufanya matokeo kuwa 1-1 ambayo yalidumu hadi dakika 90 zinamalizika.
Mechi ya leo ilikuwa ni muhimu kwa vijana wa Hans van Pluijm kupata ushindi ambao ungewapa pointi tatu na kunyanyua morali ya kufanya vizuri kwenye kundi lao.

VIKOSI VILIKUWA HIVI
Yanga SC; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua/Juma Mahadhi, Kelvin Yondani, Mtogo Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Obrey Chirwa, Amissi Tambwe/Haruna Niyonzima dk na Donald Ngoma.

Medeama FC; Daniel Adjei, Samuel Adade, Moses Sapong, Paul Adoo/Salufu Moro dk62, Daniel Amouah, Kwesi Donsu, Erick Kwakwa, Kwame Boahene, Abbas Mohamed, Bernard Ofori na Enock Atta Agyei/Malik Akowuah dk79.

Post a Comment

 
Top