0
Serikali ya Rwanda imepuzilia mbali ombi la mahakama ya kimataifa ya jinai yenye makao yake makuu huko Hague Uholanzi ICC ya kumkamata rais wa Sudan Omar al-Bashir.

Rais Bashir atahudhuria kongamano la viongozi wa Afrika linaloandalia mjini Kigali wikiendi hii.


Rais Bashir atahudhuria kongamano la viongozi wa Afrika linaloandalia mjini Kigali wikiendi hii.
Waziri wa maswala ya nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo amesema kuwa ombi la ICC kupitia kwa barua rasmi walioiandika siku mbili zilizopita haina uzito wowote.

Mapema juma hili mahakama ya ICC iliyashtaki mataifa ya Djibouti na Uganda kwa baraza kuu la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kukosa kumkamata rasi Bashir alipozuru mataifa hayo.
Hii sio mara ya kwanza ziara ya rais Bashir imezua utata.

Mwaka uliopita mahakama ya Afrika Kusini ilimpata na hatia rais Jacob Zuma kwa kukiuka amri ya mahakama ya kumtia mbarano rais Omar el Bashir alipohudhuria mkutano wa umoja wa Afrika mjini Johannesburg nchini humo.



Moja ya mada kuu katika kikao kijacho cha Kigali, itakuwa uhusiano baina ya bara la Afrika na mahakama hiyo ya ICC.
Viongozi wa Afrika wamekuwa wakishikilia kukutu dhana kuwa dhamira kuu ya mahakama hiyo ni kuwahukumu viongozi wa Afrika ,huku viongozi wa mataifa ya magharibi wakiruhusiwa kuponyoka mkono wa sheria licha ya kuwepo kwa madai dhidi yao

Post a Comment

 
Top