0
Thierry Henry ameondoka Arsenal, baada ya kukataa nafasi aliyopewa ya kufundisha wachezaji wa chini ya umri wa miaka 18.

Henry, 38, alipewa nafasi hiyo na meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ambaye alimuambia kuwa hawezi kuchanganya na kazi yake ya sasa kama mchambuzi wa soka kwenye TV.
Hata hivyo, Henry ambaye alifanya kazi na wachezaji chipukizi wa Arsenal kama sehemu ya mafunzo ya kupata leseni yake ya ukocha ya Uefa, hakuwa tayari kuacha kazi yake ya uchambuzi wa soka.
Nahodha wa zamani wa Arsenal, Tony Adams, 49, sasa atachukua nafasi hiyo ya vijana chini ya miaka 18.
Henry sasa lazima atafute timu ya kufundisha ili kukamilisha leseni yake ya ukocha.
Thierry Henry ameajiriwa na shirika la utangazaji la Sky Spors, na alifanya kazi kama mchambuzi wa BBC wakati wa michuano ya Euro 2016.

Post a Comment

 
Top