0
Mabingwa soka Tanzania bara Yanga wainatarajia kuondoka jijini Dar es salaam kwenda Ghana mwishoni mwa wiki hii kuwafuata wapinzani wao Medeama tayari kwa mchezo wa marudiano wa kuwania Kombe la Shirikisho Afrika.
Uongozi wa Timu ya Yanga unaendelea na maandalizi kwa ajili ya safari hiyo ,naye kocha mkuu wa klabu hiyo Mholanzi Hans van Der Pluijm amesema yupo tayari katika maandalizi makali kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa siku ya Jumanne ijayo, Julai 26, mwaka huu nchini Ghana.
                 
Yanga itakwenda nchini Ghana ikiwa na kumbukumbu ya kutoshana nguvu ya kufungana bao 1-1 na Medeama Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga kwa sasa inashika mkia kwenye Kundi A ikiwa na pointi moja huku TP Mazembe wakiwa kinara na pointi saba, wakifuatiwa na MO Bejaia wenye pointi tano.

Post a Comment

 
Top