0
Kipa mpya wa Simba, Aishi Manula amewasili nchini Afrika Kusini muda huu na kupokelewa na jopo la viongozi pamoja na wachezaji wenzake.
Mara baada ya kutua, Aishi alifikishwa moja kwa moja iliyo kambi ya timu  ya Simba katika hoteli ya Petra iliyopo, Edenvale, Johannesburg.
Simba iko nchini Afrika Kusini kwa kambi na leo Jumanne inatarajia kucheza mchezo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya  Orlando Pirates ya nchini humo.
Manara alisema Manula ameshamalizana kila kitu kuhusu kujiunga na  Simba na ameahidi kuwapa furaha mashabiki wa klabu hiyo sambamba na kuisaidia  kushinda mataji itakayowania msimu ujao.
Manula alisajiliwa na Simba muda mrefu, lakini klabu hiyo ilishindwa kumtangaza kutokana na kuepuka kubanwa na mkataba wa timu yake ya zamani Azam.
Hata hivyo taarifa zinadai makataba wa Azam na Manula unamalizika Agosti 10  hivyo timu hizo mbili zilikaa mezani kwa mazungumzo ili kumruhusu  mapema kipa huyo kujiunga na timu yake mpya kwa ajili ya maandalizi ya ligi.
 Simba itacheza mchezo wa kirafiki na Orlando Pirate  kesho huku ikitarajia  pia kucheza mchezo mwingine wa kirafiki Alhamisi dhidi  ya Bidvest Wist.

Post a Comment

 
Top