0

Nchi saba, ikiwemo wenyeji Uganda, watashiriki katika michuano ya Cecafa 2016 ya wanawake mwezi Septemba. Kenya, Burundi, Zanzibar, Ethiopia, Tanzania bara na Rwanda watashiriki. 

Michuano hii imethibitishwa na shirikisho la soka la Afrika Mashariki na Kati- Cecafa - mjini Kampala. Katibu mkuu wa Cecafa Nicholas Musonye amesema walitarajia kupata timu moja kutoka kusini mwa Afrika lakini hawakufanikiwa. Rais wa shirikisho la soka la Uganda Injinia Moses Magogo amesema: 
"Tumefurahi kuandaa michuano hii. Huu ni muendelezo wa mradi wa mkakati wa kukuza soka la wanawake nchini Uganda na katika eneo zima." Michuano hiyo itaanza Septemba 11 hadi 20 katika mji wa Jinja. Burundi na Zanzibar zitacheza katika mechi ya ufunguzi. makundi ni kama ifuatavyo. 


Tanzania imepangwa Kundi B pamoja na Ethiopia, Tanzania na Rwanda katika michuano ya ubingwa wa wanawake kwa mataifa ya Afrika Mashariki na Kati.

Katibu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye amewaambia Waandishi wa Habari katika mkutano wa utambulisho wa Challenge hiyo ya wanawake mjini kampala, kwamba Uganda watakuwa wenyeji wa michuano hiyo.

Katika sherehe za utambulisho wa michuano hiyo iliyofanyika makao makuu ya Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Musonye alisema nchi saba zimethibitisha kushiriki Challenge hiyo ya kwanza ya wanawake, itakayofanyika Jinja.

Mbali za Tanzania, Ethiopia na Rwanda Kundi A linaundwa na timu za Uganda, Kenya, Burundi, na Zanzibar na michuano itaanza Septemba 11 hadi 20, 2016.


Kundi A: Uganda, Kenya, Burundi, Zanzibar
Kundi B: Ethiopia, Tanzania bara, Rwanda.

Post a Comment

 
Top